Waliokufa ajali ya mashua Mto Kongo waongezeka
17 Oktoba 2023Matangazo
Hayo yalisemwa na Waziri wa Usafiri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Marc Ekila, siku ya Jumatatu (Oktoba 16).
Ripoti za awali kutoka mamlaka za jimbo la kaskazini mashariki la Equateur siku ya Jumapili (Oktoba 16) zilisema miili 28 ilikuwa imeopolewa kutoka mtoni na watu wengine kadhaa walikuwa bado hawajapatikana.
Soma zaidi: Watu 28 wafa maji Mto Kongo
Manusura waomba msaada baada ya ajali ya Meli nchini Kongo
Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu, Waziri Ekila alithibitisha idadi mpya ya vifo lakini akasema hawakufanikiwa kupata idadi kamili ya abiria waliokuwamo katika boti hiyo kutokana na utaratibu kukiukwa katika kuorodhesha abiria chomboni.