1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Waliouawa katika shambulio la ufukweni Somalia wafikia 32

3 Agosti 2024

Takriban watu watu 32 wameuawa na wengine 63 wamejeruhiwa katika shambulio la ufukweni kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Hayo yamesemwa na jeshi la polisi nchini humo mapema hii leo.

https://p.dw.com/p/4j4lo
Mogadishu
Watu wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyeuawa katika shambulizi la ufukweni katika eneo la Lido nchini SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Takriban watu watu 32 wameuawa na wengine 63 wamejeruhiwa katika shambulio la ufukweni kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Hayo yamesemwa na jeshi la polisi nchini humo mapema hii leo.  Shambulio hilo limetokea katika ufukwe maarufu wa Lido ambao hufurika mamia ya waakazi wa mji Mogadishu kwa mapumziko ya mwisho wa juma. 

Msemaji wa polisi nchini Somalia Abdifatah Aden akitoa taarifa ya tukio hilo mbele ya wandishi wa habari ameongeza kuwa mshambuliaji mmoja alijilipua mwenyewe huku wengine watatu wakiuawa na mmoja anashikiliwa akiwa hai.

Eneo hilo la Lido limekuwa likilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara, ikiwemo kisa cha wanamgambo wa Al-Shabaab kuizingira hoteli moja ya fahari mnamo mwaka 2023. Kwenye mkasa huo watu 6 waliuawa na wengine 10 walijeruhiwa.