1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Wamisionari wa Marekani wauawa nchini Haiti

25 Mei 2024

Genge la wahalifu nchini Haiti limewaua wamisionari watatu, ikiwa ni pamoja na wanandoa, raia wa Marekani, katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port au Prince.

https://p.dw.com/p/4gHB3
Wamisionari wa Marekani Davy na Natalie Lloyd waliouawa Haiti
Wamisionari wa Marekani Davy na Natalie Lloyd waliouawa HaitiPicha: Missions in Haiti/AFP

Shirika la umisionari na la hisani la Missions in Haiti, lenye makao yake kwenye jimbo la Oklahoma nchini Marekani limesema Davy na Natalie LLoyd pamoja na mkurugenzi wa shirika hilo ambaye ni raia wa Haiti Jude Montis waliuliwa na watu wenye silaha Alhamisi, usiku walipokuwa wakitoka kanisani.

Soma pia: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya inayoendelea Haiti

Baba wa Natalie ni seneta wa jimbo la Missouri, Ben Baker na Davy ni mtoto wa David na Alicia Lloyd walioanzisha shirika hilo nchini Haiti, mnamo mwaka 2000.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kisa hicho kinadhihirisha kwa mara nyingine kuwa hakuna anayeweza kuepuka vurugu nchini Haiti.