1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Wanachama 8,000 wa upinzani wakamatwa Bangladesh

5 Novemba 2023

Polisi nchini Bangladesh imewakamata takriban wanachama 8000 wa upinzani katika kamata kamata ya kitaifa tangu maafisa hao wa polisi walipousambaratisha mkusanyiko mkubwa wa upinzani mjini Dhaka wiki moja iliyopita.

https://p.dw.com/p/4YQDR
Polisi nchini Bangladesh imewakamata takriban wanachama 8,000 wa upinzani
Polisi nchini Bangladesh imewakamata takriban wanachama 8,000 wa upinzaniPicha: Munir Al Zaman/AFP

Hatua hiyo ya polisi inafanyika wakati taifa hilo likijitayarisha na uchaguzi mkuu mwezi Januari.

Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha  Bangladesh Nationalist Party (BNP) na washirika wake wamekuwa wakiandaa mikutano ya hadhara  katika miezi ya hivi karibuni, wakitaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu na kukubali serikali isiyoegemea upande wowote kusimamia masuala ya uchaguzi.

Waziri Mkuu Hasina amepata mafanikio mazuri katika uongozi wake wa miaka 15 lakini anadaiwa kuiongoza pia kimabavu nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.