Wanaharakati walinzi wa mazingira - Greenpeace Watimiza miaka 30 Ujerumani
27 Agosti 2010Tufanye amani ya ulinzi wa mazingira. Hii ndio kauli mbiu ya wanaharakati wa ulinzi wa mazingira wa Greenpeace. Katika mwaka 1997 wanaharakati wanaopigania amani walianzisha shirika hilo la Greenpeace nchini Canada. Miaka 9 baadaye , mwaka 1980, kundi la Ujerumani lilichukua uongozi. Na hii leo wanaharakati wa Greenpeace wa Ujerumani ni miongoni mwa wataalamu wanaohitajika sana kimataifa katika mtandao wa Greenpeace. Na hivi sasa tarehe 28 August greenpeace tawi la Ujerumani linasherehekea miaka 30 tangu kuasisiwa.
Kwa mara ya kwanza tunakwenda Ley West na Tortuga
Hata kama inasikika kama ni maisha ya ujasiri tu, lakini Regine Frerichs hasafiri kwa ajili ya burudani tu baharini. Mzamia mbizi huyo yuko katika ujumbe kuelekea katika ghuba ya Mexico, kama mwanachama wa kundi la wataalamu wa kimataifa wa kundi la Greenpeace, katika meli ya kundi hilo inayojulikana kama "Arctic Sunrise".
Hivi sasa mimi ndio ninawajibika, kwamba vifaa vyote vya wazamiaji hapa ni kamili.
Mara hii walinzi hawa wa mazingira wanafanya mazoezi katika eneo karibu na pwani ya Marekani ambayo haikuathirika na kumwagika kwa mafuta. Ubora wa maji kwa hivi sasa unapaswa kulinganishwa na kuchunguzwa athari za maafa hayo ya mafuta. Kutokana na uzoefu wake Regine Frerichs anaelezea katika wavuti yake katika mtandao wa internet. Wanaharakati hawana hofu, licha ya kuwa kemikali ya Corexit ambayo imetumika kusafisha mafuta hayo , inaweza kuwa ni sumu kali.
Ndio , tumejitayarisha.
Kujitayarisha na mapema hiyo ndio nguvu kuu ya Greepeace. Hata kama kuna hatari inayowakabili. Kugundua maeneo yanayoharibiwa na kutoa malalamiko. Hayo ndio linayofanya shirika hilo muhimu la ulinzi wa mazingira duniani nchini Ujerumani miaka 30 hivi sasa.
Mara zote tunakuwa katika maeneo yenye matatizo, na kulifanyia kazi moja kwa moja suala husika na hii ina maana hata mapambano ya moja kwa moja.
Hayo anayasema mmoja wa waasisi wa greenpeace nchini Ujerumani Harald Zindler akiwa pamoja na washirika wake. Kauli mbiu hiyo inaendelea hadi hii leo.
Na katika miaka hii 30 sehemu ya kundi hilo hapa Ujerumani inathibitishwa na picha kadha za upinzani waliokuwa wakiutoa duniani. Picha moja inakumbusha kampeni ya kwanza kabisa , ambayo wanaharakati wa kwanza wa greenpeace walitayarisha. Inaonyesha mtu mmoja akiwa katika bomba la kutolea maji la meli ya Kronos. Gerhard Wallmeyer, hivi leo ameiweka picha hiyo ikiashiria kuwa ni jiwe la msingi la sehemu ya kundi hilo nchini Ujerumani.
Mwanaharakati huyo wa Greenpeace ambaye alikuwa katika bomba hilo, alikuwa katika hatari , kwasababu meli hiyo ilikuwa inaondoka usiku. Na muda mfupi tu tutakuwa hatuioni tena meli hiyo. Hii ina maana hatukuwa tumejitayarisha kuendesha maboti yetu katika bahari kuu, na tulikuwa na maboti mawili ya kujaza upepo, ambayo tunayatumia kuifuata meli hiyo na tulijaribu kuizuwia kwa kutumia mataa makubwa . Mtu huyo aliingia katika meli hiyo , kwa kuwa hatukuweza kuizuwia meli hiyo na hatukuwa tumemfunga kamba. Kama sio kuwa na mataa hayo makubwa yanayowaka kuimulika meli hiyo angetupwa majini. Lakini greenpeace walifanikiwa. Meli hiyo iliweza kuzuiliwa kutokana na mzingiro ambao ulidumu muda mrefu , na shehena yake ya kemikali za viwandani ikazuiwa kwenda kutupa taka hizo katika eneo la bahari ya kaskazini.
Mwandishi : Karin Jäger / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman