1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Wanajeshi 16 wauawa katika vita vya kikabila jimbo la Delta

16 Machi 2024

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema leo kuwa askari 16 wa jeshi hilo waliuawa na makundi ya vijana mapema wiki baada ya askari hao kujaribu kuzima vita vya kikabila katika jimbo la kusini la Delta.

https://p.dw.com/p/4dnuy
Watu wakiwapita maafisa wa jeshi la Nigeria karibu na kituo cha kupigia kura katika wadi ya Kwankwaso, Kano
Watu wakiwapita maafisa wa jeshi la Nigeria karibu na kituo cha kupigia kura katika wadi ya Kwankwaso, Kano Picha: KOLA SULAIMON/AFP/Getty Images

Jenerali Tukur Gusau ameeleza katika taarifa kuwa askari hao kutoka kikosi cha 181 Amphibious kilijaribu kuzima vita kati ya jamii za Okuoma na Okoloba walipouawa na makundi ya vijana siku ya Alhamisi.

Msemaji huyo wa jeshi amesema waliouawa ni afisa mkuu, wanajeshi wawili wa cheo cha meja, nahodha mmoja na askari 12 wa kawaida.

Soma pia: Jeshi la Nigeria lawasaka waliowateka wanafunzi 300

Tayari mkuu wa majeshi Jenerali Gwabin Musa ameagiza uchunguzi wa haraka ufanyike na kukamatwa kwa wote waliohusika na vifo hivyo.

Vita vya kikabila hutokea mara kwa mara, wakati mwengine vikihusisha umwagaji damu, huku jamii nyingi za jimbo la Delta zikizozana juu ya ardhi au fidia zinazolipwa na kampuni za nishati.