Wanajeshi 250 wa Sudan Kusini waondoka Kongo
8 Desemba 2023Matangazo
Wanajeshi hao wameondoka baada ya serikali ya Kongo kukataa kurefusha muda wa kikosi hicho cha kikanda kubakia nchini humo.
Mapema leo waandishi wa shirika la habari la AFP waliwaona wanajeshi wa Sudan Kusini wakiondoka katika mji huo mkuu wa Kivu Kaskazini.
Soma zaidi: Raia wa Kongo wafurahia kuondoka wanajeshi wa Afrika Mashariki
Wanajeshi wa Uganda na Burundi pia wanatarajiwa kuondoka katika siku zijazo, huku kikosi chote cha kikanda kikitarajiwa kuondoka kabisa ifikapo Januari 7.
Kikosi cha kwanza cha kikanda kilipelekwa eneo la mashariki mwa Kongo ambalo linakumbwa na ghasia Novemba, 2022, kwa mwaliko wa viongozi wa Kongo kwa lengo la kuyakomboa maeneo yaliyochukuliwa na kundi la waasi wa M23.