1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wanajeshi wa Guatemala na El Salvador wawasili Haiti

Sylvia Mwehozi
4 Januari 2025

Zaidi ya wanajeshi 80 kutoka Guatemala na El Salvador waliwasili Haiti siku ya Ijumaa kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na Kenya.

https://p.dw.com/p/4oo9J
Haiti Port-au-Prince | Polisi wa Kenya
Polisi wa Kenya akilinda doria HaitiPicha: Jean Feguens Regala/REUTERS

Zaidi ya wanajeshi 80 kutoka Guatemala na El Salvador waliwasili Haiti siku ya Ijumaa kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na Kenya ili kuimarisha jeshi la polisi kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya kihalifu.

Hadi Kufikia sasa, kuna maafisa 400 wengi wao wakiwa Wakenya, lakini pia baadhi kutoka Jamaica na Belize kati ya 2,500 wanaotarajiwa.

Lakini kikosi hicho hakina vifaa vya kutosha huku kikijaribu kukomesha magenge yenye nguvu na yenye silaha nchini Haiti. Magenge hayo yameshutumiwa kwa mauaji, ubakaji na utekaji nyaraili kujipatia fidia.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa magenge hayo yanadhibiti takriban asilimia 85 ya mji mkuu wa Port-au-Prince. Vurugu za magenge hazijakoma katika nchi hiyo iliyokumbwa na mzozo ya Caribbean tangu jeshi la kimataifa lilipowasili.