1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Wanajeshi wa Eritrea waondoka Tigray

2 Januari 2023

Wanajeshi wa Eritrea walioisaidia serikali ya Ethiopia wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la Tigray, wameanza kuondoka.

https://p.dw.com/p/4LdBK
Äthiopien Tigray-Region | zerstörter Panzer
Picha: EDUARDO SOTERAS/AFP/Getty Images

Wanajeshi hao wa Eritrea wameanza kuondoka kutoka miji miwili mikubwa ya Shire na Axum na kuelekea mpakani.

Hayo ni kwa mujibu wa mashuhuda na afisa wa Ethiopia aliyezungumza na shirika la habari la Reuters.

Kuondoka kwa wanajeshi hao kunafuatia makubaliano ya amani ya Novemba 2 yaliyotiwa saini kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha ukombozi cha watu wa Tigray, ambapo sehemu ya makubaliano hayo ni kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni kutoka Tigray.

Eritrea hata hivyo, haikuwa sehemu ya makubaliano hayo, na uwepo wa wanajeshi wake katika jimbo la Tigray kuliibua maswali kuhusu mustakabali wa makubaliano hayo ya amani.

Hata hivyo haikubainika wazi iwapo wanajeshi wa Eritrea walikuwa wanaondoka kabisa Tigray au walikuwa wanaelekea sehemu nyengine.