Wanajeshi wanne wameuwawa katika maandamano Pakistan
26 Novemba 2024Matangazo
Wanajeshi wanne wameuwawawakati wa mapigano karibu na bunge la Pakistan kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji waliokuwa wanashinikiza kuachiliwa kutoka jela kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan.
Wizara ya mambo ya ndani ilithibitisha vifo hivyo lakini haikubainisha waliohusika, huku Waziri Mkuu Shehbaz Sharif akiwashutumu waandamanaji kwa kuwashambulia wanajeshi kwa msafara wa magari.
Katika taarifa yake Sharif amekosoa maandamano hayo akisema si ya amani na kuyataja kama ya "itikadi kali," yenye "malengo maovu ya kisiasa."
Waandamanaji hao walipora magari na kuteketeza kibanda cha polisi, huku wakitoa wito kwa serikali kuachia mamlaka miongoni mwa matakwa mengine.