1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajihadi wa Niger watoa video ya 'mateka wawili wa Urusi'

3 Agosti 2024

Kundi linalofungamana na Al Qaeda la nchini Niger limeachia video inayowaonyesha wanaume wawili waliojitambulisha kama raia wa Urusi wakisema walitekwa nyara huko Mbanga, kusini magharibi mwa Niger.

https://p.dw.com/p/4j4kb
Niger na Urusi
Bendera ya Niger na UrusiPicha: AFP/Getty Images

Kundi linalofungamana na Al Qaeda la nchini Niger limeachia video inayowaonyesha wanaume wawili waliojitambulisha kama raia wa Urusi wakisema walitekwa nyara huko Mbanga, kusini magharibi mwa Niger. 

Video hiyo inayowaonyesha wanaume hao waliojitambulisha kwa majina ya Yurit na Greg imechapishwa na kundi linalojiita Muungano wa wale wanaounga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM) ingawa haikufahamika kwamba ni lini watu hao walitekwa nyara.

Mbanga inapatikana katika eneo la Tillaberi karibu na mpaka wa Niger, Burkina Faso na Mali na migodi kadhaa ya dhahabu inapatikana eneo hilo.

Itakumbukwa kuwa Mnamo Julai 25, Urusi iliwaonya raia wake kutosafiri kwenda mataifa ya Mali na Niger kutokana na sababu za kiusalama.