Wanamgambo wauwa watu 11 karibu na Maiduguri Nigeria
28 Agosti 2019Matangazo
Waasi wanaoshirikiana na kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislam-IS wamewapiga risasi na kuwauwa wafanyakazi wa ujenzi 11 kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wengine kadhaa wamejeruhiwa. Mkuu wa wanamgambo hao na wakaazi wa eneo hilo wameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.
Waasi hao ambao ni wafuasi wa kundi la itikadi kali linalojiita "Dola la Kiislam la mkoa wa magharibi mwa Afrika SWAP waliwafyetulia risasi wafaanyakazi hao katika kijiji cha Wajirko, umbali wa kilomita 150 nje ya mji mkuu wa jimbo la Borno-Maiduguri.
Wanamgambo wa SWAP wanasemekana kuwa na ushawishi mkubwa katika katika eneo la Wajiirko na maeneo ya karibu na hapo unakokutikana msitu wa Sambisa unaodhibitiwa na kundi hasaimu la Boko Haram.