1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSierra Leone

Wananchi Sierra Leone wasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu

26 Juni 2023

Wananchi wa Sierra Leone wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, bunge na serikali ya mitaa, uliofanyika Jumamosi huku upinzani ukitowa madai kwamba hakuna uwazi katika zowezi hilo.

https://p.dw.com/p/4T3io
Sierra Leone | Präsidentschafts- und Parlamentswahlen | Stimmabgabe
Picha: John Wessels/AFP/Getty Images

Shughuli ya kukusanya matokeo kwenye vituo vya kupigia kura inaendelea katika ngazi ya mikoa. Mkuu wa tume ya uchaguzi Mohammed Konneh jana jumapili alisema uchaguzi wa mwaka huu ni mmoja kati ya chaguzi nzuri zilizowahi kufanyika katika historia ya nchi hiyo.

Soma pia: Raia wa Sierra Leone wanapiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani.

Matokeo yalitarajiwa kutangazwa ndani ya saa 48 baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika. Hata hivyo mgombea urais wa chama cha upinzani cha All Peoples Congress APC Samura Kamara amedai kwamba tume ya uchaguzi inawazuia pamoja na vyama vingine vya kisiasa kulinganisha na kuthibitisha zoezi la ukusanyaji na ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi.

Kwa wiki kadhaa sasa chama hicho kimekuwa kikilalamikia juu ya upendeleo unaofanywa na tume ya uchaguzi. Samura Kamara ndio mpinzani wa karibu anayepambana kumuondowa  rais  Julius Maada Bio.