Wananchi wa Algeria wapiga kura leo
17 Aprili 2014Vituo vya kupiga kura vilifungulia tangu saa mbili asubuhi saa za Algeria kwa ajili ya zoezi hilo litakaloendelea kwa saa 11 zijazo. Wagombea wakuu katika uchaguzi huo ni rais wa sasa Abdel Aziz Boutefilika mwenye umri wa miaka 77 ambaye anagombea muhula wa nne licha ya afya yake kuwa mbaya na aliyekuwa waziri mkuu Ali Benflis mwenye umri wa miaka 69 ambaye anatajwa huenda akampa changamoto Bouteflika katika uchaguzi huu. Je wachambuzi wa mambo wanautazama vipi uchaguzi huu hasa ikizingatiwa mara zote nchini Algeria chaguzi zinakumbwa na utata na madai ya udanganyifu. Saumu Mwasimba amezungumza na Ahmed Rajab mchambuzi wa Kimataifa. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri:Josephat Charo