Wanasheria wataka Mahakama ya Juu kumshitaki Trump
9 Aprili 2024Taarifa ya waendesha mashitaka hao iliwasilishwa usiku wa kuamkia Jumanne (Aprili 9) kwenye Mahakama ya Washington, ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya majaji kuamua endapo rais huyo huyo wa zamani ashitakiwe ama ala kwa kile alichokitenda wakati akiwa kwenye Ikulu ya White House.
Soma zaidi: Trump aendelea kuisaka kinga dhidi ya makosa yanayomkabili
Wanasheria hao waliiandikia mahakama kwamba njama ya Trump kutaka kutumia madaraka yake kubadili matokeo ya uchaguzi na kuhujumu makabidhiano ya madaraka yalikuwa mambo yanayokinzana kabisa na vifungu vya katiba vinavyoilinda demokrasia ya Marekani.
Uamuzi wa mwisho unatarajiwa tarehe 25 mwezi huu wa Aprili na ndio utakaotowa muelekeo wa kesi hiyo dhidi ya Trump, ikiwa ni takribani miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu, ambao bilionea huyo wa chama cha Republican anatazamiwa kuchuwana tena na Joe Biden wa Democrat.