SiasaIran
Narges Mohammadi ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel
6 Oktoba 2023Matangazo
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel Berit Reiss-Andersen, akimtangaza mshindi wa tuzo hiyo mjini Oslo leo amesema Narges Mohammadi, ametunukiwa kwa ujasiri wake wa kupigania haki na kupinga ukandamizaji wa wanawake nchini mwake.
Mohammadi ni miongoni mwa wanaharakati wanawake wa Iran ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki nchini humo baada ya kisa kilichohusisha kifo kilichotokea mikononi mwa polisi, cha msichana, Mahsa Amin aliyekamatwa kwa kukiuka sheria kali ya mavazi ya wanawake nchini humo.
Jumla ya watu 351 ikiwa ni pamoja na mashirika mbalimbali ni miongoni mwa walioteuliwa kushindania tuzo hiyo mwaka huu.