1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake Saudia Arabia sasa kutengamana na wanaume

Babu Abdalla9 Desemba 2019

Wanawake Saudia Arabia hawatahitajika tena kutumia milango tofauti na wanaume ama hata kukaa sehemu tofauti katika migahawa iliyotenganishwa na wanaume. Hizi ni hatua za hivi karibuni zilizotangazwa na serikali. 

https://p.dw.com/p/3UU94
Saudi-Arabien Aziza al-Yousef
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Jamali

Hatua hizi mpya ambazo zilitangazwa mnamo Jumapili na Wizara inayohusika na manispaa na serikali za vijiji ya Saudia Arabia zinaonekana kama ushindi kwa wanawake nchini humo. Ni uamuzi ambao unaonekana kuondoa vizuizi vya ubaguzi hasa kwa wanawake.

Licha ya uamuzi huo kutolewa Jumapili, bila kujali sheria za hapo awali migahawa mengine iliyoko katika mji wa Pwani wa Jiddah na Riyadh tayari ilikuwa inaruhusu wanaume na wanawake wasio na uhusiano wa kindugu kukaa huru na kutengamana bila wasiwasi.

Hata hivyo, uamuzi wa kuwaruhusu wanawake na wanaume wasio na uhusiano umeonakana kama suala lililopitwa na wakati ambapo wahafidhina waliona kama mwiko utengamano wa wanaume na wanawake wasio ndugu.

Katika hatua ya kushangaza, nchi jirani za Kiislamu zinazopakana na Saudia Arabia hazikuwa na sheria kama hizo za kuzuia wanaume na wanawake kukaa huru.

Loujain al-Hathloul
Mwanamke akiendesha gariPicha: picture-alliance/AP Photo/Loujain al-Hathloul

Limekuwa jambo la kawaida nchini Saudia Arabia, kwa wanaume na wanawake ambao hawana uhusiano wa karibu kuruhusiwa kuchanganyika katika sehemu za umma.

Sio sehemu za umma pekee, bali shule zinazoendeshwa na serikali, vyuo vikuu na hata harusini pia wanaume na wanawake hawaruhisi kuchanganyika.

Yamkini migahawa nchini Saudi Arabia, ikiwemo ile inayomilikiwa na watu kutoka sehemu nyengine duniani kama vile Starbucks pia imetenga sehemu maalum za familia, wanawake walio pekee yao, na wanaume ambao bado hawajaoa.

Migahawa hiyo pia ina milango tofauti ya wanawake na wanaume, vyumba vya familia ambavyo wanawake hawaoekani na wanaume. Na wakati mwengine hasa kwenye mikahawa midogo ama isiyo na nafasi ya kutenga wanaume na wanawake, wanawake hawarusihi kabisa kuingia.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mfalme Mohammed bin Salman amekuwa akifanya mabadiliko ya kijamii kwa kuruhusu wanaume na wanawake kuhudhuria matamasha na sinema ambazo hapo awali zilikuwa zimepigwa marufuku. Pia alipunguza nguvu ya polisi ambayo ilikuwa na jukumu la kuhakikisha sheria za kihafidhina zinatekelezwa ikiwemo kuwatenganisha wanaume na wanawake katika sehemu za umma.

Miaka miwili iliyopita, kwa mara ya kwanza wanawake waliruhusiwa kuhudhuria michezo katika viwanja mbalimbali vya michezo katika sehemu zilizotengwa kwa ajili ya familia huku nao wasichana wakiruhusiwa kushiriki michezo shuleni, haki ambayo ilikuwa imepewa wavulana pekee.

Saudi-Arabien erste Frauen mit Führerschein
Mwanamke wa Saudia akionyesha leseni ya uderevaPicha: picture-alliance/AP Photo/Saudi Information Ministry

Mnamo mwezi Agosti, mamlaka nchini humo iliondoa marufuku ya usafiri kwa kuwaruhusu raia wote wakiwemo wanawake na wanaume kuomba hati ya kusafiria na kusafiri wakiwa huru hadi mataifa ya nje. Marufuku hiyo iliyokuwepo kwa muda mrefu ililenga kudhibiti uhuru wa wanawake kusafiri bila ya kuwepo kwa mwanaume msimamizi.

Mamlaka nchini humo iliondoa marufuku ya wanawake kujiendesha wenyewe ambayo ilifikia ukomo wake mwaka 2018 iliyokuwa imedumu kwa miongo kadhaa

Mamlaka nchini humo imesema kuwa uamuzi wa kuondoa sheria hizo za kihafidhina unalenga kuvutia wawekezaji zaidi na kufungua fursa za biashara.

Hata hivyo, ingawa serikali imetangaza kuondolewa kwa vizuizi hivyo, sio wote wanaofurahia uamuzi huo kwani bado wako watu ambao wanaendelea kuzifuata sheria hizo za kihafidhina za kutowaruhusu wanaume na wanawake ambao hawana uhusiano kuchanganyika.

Familia nyingi za kihafidhina bado zinapendelea kula katika migahawa yenye sehemu maalum za wanawake na wanaume huku wanawake wakifunika nyuso zao na kuvaa hijab - kitambaa kinachovaliwa kichwani na wanawake wa Kiislamu katika sehemu za umma.