1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Miaka 30 ya mauaji ya kimbari yakumbukwa Kigali

7 Aprili 2024

Wanyarwanda wanakumbuka mauaji ya kimbari yaliyotokea miaka 30 iliyopita, yaliyopangwa na Wahutu wenye msimamo mkali dhidi ya jamii ya Watutsi.

https://p.dw.com/p/4eVwP
Rwanda 1994
Jumba la kumbukumbu la mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Ukatili huo uliofanyika kwa siku 100 kabla ya  jeshi la waasi la Rwandan Patriotic Front (RPF) kuwashinda Wahutu wenye itikadi kali mwezi Julai mwaka 1994, ulisababisha vifo vya watu 800,000 wengi wao kutoka jamii ya watutsi na wahutu waliojaribu kuwalinda. 

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameuwasha mwenge katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, kuwakumbuka wahanga wa mauji hayo yaliyotokea Aprili 7 mwaka 1994. Kagame pia ameweka mashada ya maua katika makaburi ya halaiki katika kumbukumbu hiyo inayohudhuriwa na wanadiplomasia na viongozi wa kigeni akiwemo rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. 

Wanyarwanda wakumbuka miaka 30 ya mauaji ya kimbari

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kutoa ujumbe siku ya leo akisema Ufaransa na washirika wake wa Magharibi na Afrika wangeliweza kuyazuia mauaji hayo lakini walikosa ari ya kufanya hivyo.