1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Wapalestina 17 wauawa kufuatia shambulio la Israel Gaza

1 Januari 2025

Wapalestina 17 wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Bureji na mji wa Jabalia, kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ojDd
Gaza | Deir Al-Balah | Al-Magasi
Wapalestina waliojeruhiwa katika shambulio la Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi katika mkoa wa Deir Al-BalahPicha: Adel Al Hwajre/picture alliance/ZUMAPRESS

Hayo yameripotiwa na shirika rasmi la habari la mamlaka ya Palestina, WAFA.

Jeshi la Israel IDF hata hivyo halijazungumzia juu ya shambulio hilo japo kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji wake aliwaonya wakaazi wa al-Bureij kuondoka kutokana na uwezekano wa Israel kulishambulia eneo hilo ili kulenga wanamgambo waliokuwa wakifyetua roketi kutoka eneo hilo.

Soma pia: Wanajeshi wa Israel wavamia na kuchoma hospitali Gaza 

Jeshi hilo la IDF limesema limemuua usiku wa kuamkia leo Abd al-Hadi Sabah, mwanachama wa Hamas aliyesaidia kuongoza uvamizi katika ardhi ya Israel wakati wa shambulio la Oktoba 7, mwaka 2023 lililofanywa na wanamgambo wa Hamas.