1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina zaidi ya 20,000 wauwawa tangu kuzuka vita

Hawa Bihoga
22 Desemba 2023

Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza, imesema zaidi ya Wapalestina 20,000 wameuwa katika mashambulizi ya Israel, huku Umoja wa Mataifa ukionya watu nusu milioni wanakabiliwa na njaa.

https://p.dw.com/p/4aTbG
Ukanda wa Gaza | Mwathirika mashambulizi ya Israel akiingizwa katika gari la wagonjwa.
Waathirika wa mashambulizi ya mambomu ya Israel wakiimgizwa katika gari la wagonjwa kupelekwa hospitalini kwa matibabuPicha: MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images

Idadi hiyo ya vifo vya zaidi ya watu 20,000 ni takriban asilimia moja ya idadi ya watu  wa Gaza kabla ya kuzuka kwa vita hivyo. Hiyo ni mojawapo ya kipimo cha uharibifu uliotokana na mzozo huo ambao kwa muda wa wiki 11 sasa umesababisha karibu asilimia 85 ya wakaazi wa Gaza kuyakimbia makaazi yao.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliotolewa siku ya Alhamisi takribani watu nusu milioni, sawa na robo ya idadi jumla ya wakaazi wanakabiliwa na njaa ikiwa ni matokeo ya mashambulio ya mabomu na mzingiro wa vikosi vya Israel katika eneo hilo.

Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa mataifa Martin Griffiths aliandika katika mtandao wake wa X zamani ukijulikana Twitter kwamba, kuruhusiwa kuendelea kwa mzozo huo wa kikatili licha ya matokeo ya kimwili, kiakili na uharibifu mkubwa unaoshuhudiwalimebaki kuwa ni doa lisilofutikalicha ya dhamira ya pamoja iliopo.

Soma pia:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura juu ya rasimu mpya ya kutaka kusimamishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza

Licha ya udharura wa kushughulikia mzozo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana Alhamisi jioni lilichelewesha tena zoezi la upigaji kura juu ya ufikishwaji wa misaada ya kiutu na masharti ya usitishwaji mapigano baada ya majadiliano mapana kwa siku za nyuma. Marekani ambayo ina nguvu ya kura ya turufu imerudi nyuma dhidi ya usitishwaji wa mapigano.

Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield anasema azimio kuhusu Gaza limeandaliwa ambalo Marekani inaweza kuunga mkono katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni kuruhusu misaada ya kiutu.

"Tupo tayari kupiga kura. lakini ni azimio ambalo litaleta misaada ya kibinadamu kwa wale ambao wanauhitaji."

Alisema mwakilishi huyo wa marekani akisema kuwa Washington itaunga mkono kipaumbele ambacho Misri inacho katika kuhakikisha kwamba kunakuwepo utaratibu katika eneo hilo ambao utasaidia ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu.

"Tupo tayari kupiga kura kwa hilo." Aliwaambia waandishi wa habari.

Israel yaongeza mashambulizi

Licha ya miito ya kimataifa ya kusitishwa kwa mapigano, Israel imeapa kuendelea na mashambulizi hadi pale kundi la wanamgamo la Hamas ambalo limetawala Gaza kwa kipindi cha miaka 16 litakapoangamizwa.

Makubaliano ya kusitisha vita Israel-Hamas kurefushwa?

Jeshi hilo limesema hapo jana Alkhamis kwamba linatuma vikosi vya ardhini katika mji wa Khan Younis kwa ajili ya kuwalenga wanamgambo wa Hamas ambao wanadhaniwa kujificha katika mahandaki.

Kampeni yaIsrael ya angani na ardhiniimeelekezwa zaidi katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza eneo lililokuwa na wakaazi takriban milioni 2.3 ambao wengi wao waliyahama makaazi yao mwanzoni kabisa mwa vita, ambapo tangu wakati huo vikosi vya Israel vimekuwa vikiongeza mashambulizi yake katika mji wa Khan Younis ambao ni wapili kwa ukubwa.

Soma pia:Raia wa Gaza wanakabiliwa na hali mbaya ya kiutu kutokana na mashambulizi yanayoendelea na yaliyosababisha uharibifu mkubwa

Wizara ya afya Gaza imesema leo Ijumaa kwambaimerekodi vifo 20,057 tangu kuzuka kwa vita hivyo. hata hivyo ripoti hiyo haikutofautisha wapiganaji na raia wakawaida.

Hapo awali wizara hiyo ilisema kwamba takriban theluthi mbili ya waliokufa walikuwa wanawake na watoto na Wapalestina wengine 53,320 wamelijeruhiwa.