Wapiganaji wa kundi la Wagner wajiandaa kuondoka Bakhmut
22 Mei 2023Kiongozi huyo wa Wagner amesema watakukabidhi majukumu kwa jeshi la Urusi, baada ya kundi hilo kudai limeudhibiti kikamilifu mji huo. Wapiganaji hao pamoja na jeshi la Urusi wote wamesema mji wa Bakhmut uko mikononi mwao, ingawa serikali ya Ukraine mjini Kiev imekanusha madai hayo ikisema bado wanajeshi wake wako kwenye mji huo na mapambano yanaendelea.
Kiongozi wa kundi la Wagner amesema wapiganaji wake wamekwishaweka eneo la ulinzi katika vitongoji kadhaa katika eneo la Magharibi mwa mji huo kabla ya mpango huo wa kukabidhi majukumu kwa jeshi la Urusi.
Soma pia: Kundi la Wagner ladai kuudhibiti mji wa Bakhmut
Hatua ya kuondoka wapiganaji hao kwa mujibu wa Prighozin itaanza Mei 25 mpaka Juni Mosi. Rais Vladimir Putin amelipongeza kundi hilo la Wagner na wanajeshi wa nchi yake kufuatia madai ya ushindi huo.