1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Wapinzani Nigeria ´waukalia kooni´ushindi wa rais Tinubu

20 Septemba 2023

Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais uliofanyika mapamea mwaka huu nchini Nigeria wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliothibitisha ushindi wa rais Bola Tinubu.

https://p.dw.com/p/4WZxD
Waliokuwa wagombea wakuu wa uchaguzi wa Nigeria mnamo mwezi Februari. Kutoka kushoto ni Peter Obi, Bola Tinubu na Atiku Abubakar.
Waliokuwa wagombea wakuu wa uchaguzi wa Nigeria mnamo mwezi Februari. Kutoka kushoto ni Peter Obi, Bola Tinubu na Atiku Abubakar.Picha: K. Gänsler/DW, Shengolpixs/IMAGO, EKPEI/AFP

Katika rufaa mbili tofauti zilitowasilishwa mbele ya Mahakama ya Juu ya nchi hiyo, wagombea hao Atiku Abubakar na Peter Obi wanaomba kutangazwa kuwa washindi badala ya rais Tinubu.

Nyaraka za mahakama zinaonesha wanasiasa hao wawili wote wanalalamika kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama mapema mwezi huu wa kukataa kesi zao za awali za kuupinga ushindi wa Tinubu, ulipuuza ushahidi ulioonesha dosari za uchaguzi ambao ulifanyika mwezi Februari.

Kwenye uchaguzi huo Atiku wa chama cha Peoples Democratic (PDP) alishika nafasi ya pili na Obi wa Labour Party alikuwa mshindi wa tatu.