Wapinzani Uingereza wakimbilia mahakamani kumpinga Boris
29 Agosti 2019Uamuzi wa Jonhson umeitikisa sehemu kubwa ya nchi hiyo na kusababisha kujiuzulu mwanasiasa mashuhuri wa kihafidhina Ruth Davidson. Ruth Davidson, mhafidhina anaeunga mkono Uingereza iendelee kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ameutaja "mzozo wa Brexit" katika barua yake ya kujiuzulu na kumsihi Boris Johnson asake uwanja wa masikilizano pamoja na Umoja wa Ulaya.
Mwanasiasa huyo mwenye haiba amefanikiwa kukipatia upya umaarufu chama cha kihafidhina katika jimbo la Scottland ambalo analiongoza tangu mwaka 2011.
Uamuzi wa Boris Johnson wa kusitisha shughuli za bunge kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa september hadi October 14, wiki mbili kabla ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa ulaya umezusha ghadhabu na fadhaa nchini Uingereza ngome ya mfumo wa kimambo leo wa bunge.
Boris Johnson anasema anataka kuutumia muda huo ili kubuni sera mpya kwaajili ya nchi hiyo. Lakini upande wa upinzani unauangalia uamuzi wa waziri mkuu kuwa ni mbinu ya kuwazuwia wabunge wasipinge dhamiri ya serikali ya kuitoa nchi hiyo katika Umoja wa ulaya ifikapo October 31 inayokuja hata bila ya kupatikana makubaliano.
"Hakuna mfano wowote katika historia ya hivi karibuni ambapo bunge linazauwiliwa namna hivi" amelalamika Gina Miller, tajiri mmoja wa kile ambae ni mmojawapo wa wanaharakati wanaopinga kujitoa Uingereza katika umoja wa ulaya na ambae ametuma malalamiko yake mahakamani nchini humo. Katika mahojiano na BBC Gina Miller anahoji uamuzi wa waaziri mkuu umeölengwa kulizuwia bunge lisipitishe sheria dhidi ya ukosefu wa makubaliano.
Alikuwa mfanyabiashara huyo huyo aliyetuma malalamiko yake mahakamani mwaka 2017 kuilazim isha serikali ya wakati ule iliyokuwa ikiongozwa na Theresa May ishauriane na bunge kuhusu mango wa kujitoa Uingereza katika umoja wa ulaya.
Na kundi la wabunge 75 wanaoelemea upande wa Umoja wa Ulaya wameomba wasikilizwe na mahakama kuu ya Scotland September sita inayokuja.
Wakati huo huo mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya Brexit, Michel Barnier amemuonya waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson Umoja wa Ulaya utaenfdelea kutetea massilahi ya wananchi na makampuni yake sawa na masharti ya usalama na utulivu katika kisiwa cha Ireland.