Wapinzani wamtaka mwenyekiti wa IEBC kujiuzulu
6 Julai 2022wagombea hayo wametoa kauli hiyo ikiwa zimesalia siku 33 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, huku suala la karatasi za kura ya urais likiendelea kugubikwa na kiwingu.
Muungano wa Thirdway Alliance ulimtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, Wafula Chebukati, kujizulu na shughuli ya kuchapisha makaratasi ya kumpigia kura rais kusitishwa.
Haya yanajiri baada ya mahakama kuu kuamuru kuwa kigezo cha kuwataka wagombea kuwa na nakala za vitambulisho vya taifa vya wafuasi kutokea kaunti zisizopungua 24 kinakiuka katiba.
Kwa mtazamo wake Dr Ekuru Aukot anayeuongoza muungano wa Thirdway Alliance,mchakato uliowapa nafasi wagombea wanne pekee wa urais katika uchaguzi ujao ulikiuka sheria.
"Mahakama kuu imekwisha aamua labda rufaa ikatwe" Alisema Aukot na kuongeza kuwa uchaguzi ni mchakato hivyo Wafula na timu yake inapaswa kujitafakari.
Waliobwagwa waunga mkono hoja.
Kauli za kutaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kuingia kwenye uchaguzi mkuu mnamo mwezi Agasti Wafula Chebukati, zinazidi kushamiri kwa tuhuma za kukosa uadilifu.
Reuben Kigame wa chama cha Federal ambaye pia alibwagwa na IEBC katika harakati za kutaka kuwania urais ifikapo Agosti aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo kijiuzulu.
Soma Pia:IEBC yatoa mafunzo kwa waandishi kuelekea uchaguzi
Alisema muungwana anayo nafasi ya kujitafakari akiwa kando ya taasisi hiyo nyeti, hivyo ni wakati mujarabu kwa wafura kuachia ngazi.
"Wafula i wakati wa kujiondoa sababu amekuwa ni aibu kwenye tume" alisema mwanasiasa huyo ambae hatashiriki kuwania nafasi ya urais.
Wafula:IEBC inatafari uamuzi wa mahakama
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chabukati alisema wanatathmini uamuzi wa mahakama na watatoa jibu kamili kwa wakati.
Kisheria, IEBC inaweza kukata rufaa,kuomba ushauri wa mahakama iwapo wataandaa mchakato mpya wa kuwateua wagombea wa urais au kuutupilia mbali na kusubiri agizo jipya la moja kwa moja.
Hata hivyo, kambi ya Azimio la Umoja One Kenya inadai kuwa wapinzani wake wa muungano wa Kenya Kwanza wanapanga njama ya kuutia hila uchaguzi mkuu.
Soma pia:Kenya: Wadau wasisitiza amani katika uchaguzi Kisumu
Hoja hiyo wanaipa nguvu kwa kuhusisha uhusiano wa karibu kati ya Azimio la Umoja One Kenya na kampuni ya Ugiriki iliyopewa kandarasi ya kuchapisha makataratasi ya kupigia kura.
Inadaiwa kuwa viongozi wa kampuni hiyo walialikwa na mshirika wa mkuu wa Kenya Kwanza Moses Wetangulakuja kuzungumzia nafasi za uwekezaji.
Seneta huyo wa Bungoma anakanusha madai hayo. Zimesalia siku 33 kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti na kampeni zimeshika kasi.