1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush atangaza vikwazo zaidi dhidi ya Burma

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EM

Rais George W.Bush wa Marekani ametangaza vikwazo vikali zaidi dhidi ya utawala wa kijeshi wa Burma kwa sababu ya ukandamizaji wa kisiasa unaoendelea katika nchi hiyo ya Asia.Vikwazo hivyo hasa vitawalenga viongozi darzeni kadhaa wa utawala huo wa kijeshi.

Bush katika hotuba yake ametoa mwito kwa China na India kuushinikiza zaidi utawala wa kijeshi wa Burma.Mwezi uliopita,Ikulu ya Marekani iliweka vikwazo dhidi ya maafisa 14 wa utawala huo wa kijeshi na mali za baadhi ya viongozi hao, zimezuiliwa na seraikali ya Marekani.