1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush aunga mkono juhudi za Ukraine kuingia WTO

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQB

Rais George W.Bush wa Marekani amesema ataiunga mkono juhudi ya Ukraine kutaka kuingia katika Shirika la Biashara la Kimataifa-WTO.Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Washington akiwa pamoja na rais Viktor Yushchenko wa Ukraine,rais Bush alisema atalishinikiza Baraza la Congress la Marekani kuondoa vikwazo vya biashara dhidi ya nchi hiyo ambayo hapo zamani ilikuwa jamhuri mojawapo ya Soviet Union.Bush pia akasema anaelewa kuwa Yushchenko wakati wa kampeni ya uchaguzi alitoa ahadi ya kuvirejesha nyumbani vikosi vya Ukraine kutoka Iraq.Inatazamiwa kuwa hadi mwezi wa Septemba vikosi vyote vitaondoka Iraq.Rais wa Ukraine amesema lakini yupo tayari kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Iraq.Uhusiano wa Ukraine na Marekani umeimarika tangu Yushchenko anaeelemea upande wa magharibi,kushika madaraka mwezi wa Januari.Rais Yushchenko yupo Marekani kwa ziara ya siku tano.