1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Iran haitopingwa kuingia WTO

12 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXn

Marekani ipo tayari kutoa vichecheo vya kiuchumi ili Iran iachilie mbali miradi yake ya kinuklia.Serikali ya Washington imesema haitopinga ombi la Iran kutaka kujiunga katika Shirika la Biashara Duniani-WTO.Maafisa wa Kimarekani vile vile wamesema kuwa watafikiria kuiruhusu Iran kununua vipuri vya ndege za abiria.Na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice amesema lengo la vichecheo ni kusaidia juhudi za kidiplomasia za nchi za Ulaya zinazojadiliana na serikali ya Iran zikiitaka isitishe mpango wa kutengeneza silaha za kinuklia,ikishukiwa kuwa Iran ina azma ya kutengeneza silaha hizo.Iran imepuza ahadi zilizotolewa na Marekani kuwa hazina maana.