1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Korea Kaskazini yazidi kushinikizwa

24 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFU4

Rais George W Bush wa Marekani ameitaka Korea Kaskazini kurudi kwenye mazungumzo ya nchi sita juu ya mpango wake wa nuklea kwa matlaba ya amani na utulivu na hiyo kuongezea shinikizo kwa serikali hiyo ya Pyongyang kutoka kwa rafiki yake mkuu China kurudi kwenye mazungumo hayo.

Bush alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari hapo jana baada ya waziri wa mambo ya nje Condoleezza Rice kurudi kutoka ziara ya Asia ambapo kwayo alisema serikali ya Marekani haitoweza kusubiri maisha kwa Korea Kaskazini kurudi kwenye mazungumzo hayo.

Hata hivyo Bush amekanusha kwamba ameweka mwezi wa Juni kuwa ni wa mwisho kwa kuanzishwa tena mazungumzo hayo kwa kusema kwamba mataifa matano ambayo yamekuwa yakizungumza na Korea Kaskazini ambayo ni Marekani,China, Japani,Korea Kusini na Russia yako kitu kimoja katika kutaka Korea Kaskazini irudi kwenye mazungumzo hayo.

Bush amekaririwa akisema yeye ni mtu wa subira pamoja na watu wengi wanaohusika na suala hilo na kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini lazima afahamu kuwa wakati mataifa matano yanapotamka huwa yanakusudia kile inachosema.