WASHINGTON: Marekani itaendelea kuishinikiza Burma
28 Septemba 2007Matangazo
Marekani imezuia mali ya maafisa waandalizi 14 wa Burma,baada ya serikali ya kijeshi kutumia nguvu kukandamiza maandamano ya amani.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice alipozungumza katika Umoja wa Mataifa mjini New York, alisisitiza kuwa Washington itaendelea kuishinikiza serikali ya Rangoon.Wakati huo huo, Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa mwito kwa China, iliyo mshirika wa Burma,kujiunga na wanachama wengine wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kulaani ukandamizaji nchini Burma.