1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani na Japani zajadili Korea Kaskazini

20 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFcO

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condollezza Rice na Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld wamekutana na mawaziri wenzao wa Japani mjini Washington kujadili mpango wa nuklea wa Korea Kaskazini.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo imeelezea kufadhaishwa na tangazo la Korea Kaskazini la terehe 10 mwezi wa Februari kwamba tayari nchi hiyo imetengeneza mabomu ya nuklea.Rice amesema kushiriki kwa serikali ya Korea Kaskazini kwa kurudi tena kwenye mazungumzo ya nchi sita ni njia pekee ya kufanikisha ushirikiano mzuri wa kimataifa.

Repoti kutoka shirika la habari la serikali ya China imemkariri msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea Kaskazini ambaye hakutajwa jina akisema kwamba Korea Kaskazini haina tena utashi wa kukutana ana kwa ana na maafisa wa serikali ya Marekani na wala haitorudi kwenye mazungumzo hayo yanaozishirikisha nchi sita.