WASHINGTON: Tatizo ni kunyimwa haki na amani katika Palestina
8 Machi 2007Matangazo
Mfalme Abdullah wa Jordan ametoa wito kwa Marekani ichukue hatua ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina.Akihotubia mabaraza yote mawili ya bunge la Marekani mjini Washington,Mfalme Abdullah alisema,Marekani ndio yenye ufunguo wa upatanisho kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati.Tatizo kubwa la kanda hiyo si vita vya Irak,bali ni kule kunyimwa haki na amani katika Palestina.Mfalme Abdullah akaongezea kuwa Wapalestina leo hii wanaishi katika hali ya kuvunjika moyo na isiyo na matumaini.