WASHINGTON : Urusi yaridhiwa kuwa mwanachama wa WTO
11 Novemba 2006Marekani na Urusi zimefikia makubaliano kimsingi ambapo serikali ya Marekani itaidhinisha kujiunga kwa Urusi katika Shirika la Biashara Duniani WTO.
Maafisa wa Marekani na Urusi wamesema bado ingali kuna mambo yanayohitaji kukamilishwa lakini makubaliano hayo yatatiwa saini kwenye mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia na Pasifiki utaokafanyika mjini Hanoi nchini Vietnam wiki ijayo.Urusi ni nchi pekee yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani ambayo hadi sasa sio mwanachama wa shirika hilo.
Kikwazo kikuu katika mazungumzo ya nchi hizo mbili ni suala la nyama ya Marekani kuingizwa Urusi.
Marekani pia imekuwa ikishinikiza sana juu ya suala la kulinda haki miliki na kupatiwa nafasi katika masoko ya huduma za fedha nchini Urusi.