WASHINGTON:Rais Bush aahidi kutoa dolla milioni 50 kwa Palestina
27 Mei 2005Rais Goerge W Bush wa Marekani amemuhakikishia rais Mahmoud Abbas wa Palestina kwamba anamuunga mkono katika kuunda dola la wapalestina.
Katika mkutano wa ikulu ya Marekani rais Bush pia ameahidi kutoa kiasi cha dolla milioni hamsini kuisaidia Palestina kujijenga upya baada ya kukamilika kwa mpango wa Israel wa kuyahama maeneo ya wapalestina katika ukanda wa Gaza pindi mwezi wa Agosti.
Wakati huo huo rais Bush amempongeza kiongozi huyo wa wapalestina kwa kuchagua njia ya amani kuelekea kuunda dola la wapalestina na hatua yake ya kutafuta suluhisho la mzozo kati ya wanamgambo wa kipalestina na waisrael.
Hata hivyo rais Mahmoud Abbas upande wake amelalamika kuhusu hatua ya waisrael ya kuendelea kuyakalia maeneo ya wapalestina.
Rais Bush ameitaka Israel kukomesha ujenzi wa makazi yao katika maeneo ya wapalestina na kuitolea wito kufuata mpango wa amani wa Road Map.