WASHINGTON:Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kukztana na rais Bush katika Ikulu ya Marekani
26 Mei 2005Matangazo
Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ameitaka Marekani kujitolea katika kuisaidia Palestina kuunda dola lake.
Rais Abbas yupo nchini Marekani kwa ajili ya mazungumzo na rais Gorge Bush katika ikulu ya Marekani baadae hii leo.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Palestina kuwahi kufanya ziara kama hii tangu kusambaratika kwa mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati miaka mitano iliyopita.
Hapo jana rais Mahmoud Abbs alikutana na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Marekani akiwemo makamu wa rais Dick Cheney.