1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washirika wa Magharibi waulalamikia uchaguzi wa Hong Kong

Zainab Aziz Mhariri: Daniel Gakuba
20 Desemba 2021

Marekani,Uingereza na Australia zimeelezea wasiwasi juu ya bunge jipya la jiji la Hong Kong kutokana na sheria zilizotumika katika uchaguzi. China imeweka sheria mpya kwenye jiji hilo tangu kuchukua mamlaka mwaka 1997.

https://p.dw.com/p/44aWc
Parlamentswahl in Hongkong
Picha: Tyrone Siu/REUTERS

China imekuwa inawaandama wapinzani baada ya jiji hilo la Hong Kong kukumbwa na maandamano  makubwa ya kutetea demokrasia mnamo mwaka 2019. China imeweka sheria ya kulinda usalama wa taifa inayonyamazisha sauti za wapinzani. Sheria hizo zinawapendelea watiifu wa China ambao wanaruhusiwa kusimama katika uchaguzi.

Uchaguzi wa kwanza chini ya sheria hizo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Magharibi ikiwa pamoja na Marekani na Canada wameeleza wasiwasi mkubwa juu ya kumomonyoka kwa demokrasia katika mfumo wa uchaguzi kwenye jimbo la Hong Kong. Kulingana na sheria za sasa idadi ya wajumbe wanaochaguliwa moja kwa moja kuingia bungeni zimeondoa upinzani wa kuaminika.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Huang Jingwen/Xinhua/picture alliance

Katika tamko lao mawaziri wa nchi za magharibi wamesema wana wasi wasi mkubwa juu ya athari  zilizosababishwa na sheria ya usalama wa taifa iliyowekwa kwenye jiji la Hong Kong na juu ya kuongeza kwa hatua za kubana uhuru wa kutoa maoni na kubanwa kwa uhuru wa mikutano. Jumuiya za kiraia zimekumbwa na athari hizo.

Katika uchaguzi wa bunge la Hong Kong wa Jumapili iliyopita wajumbe ambao ni watiifu wa chama cha kikomunisti cha China walishinda kwa kishindo. Wajumbe wanaotetea demokrasia hawakuweza  kushiriki kutokana na kufungwa jela.

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam
Kiongozi wa Hong Kong Carrie LamPicha: Tyrone Siu/REUTERS

Hata hivyo kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema ameridhishwa na matokeo ya uchaguzi licha ya idadi ya wapiga kura kufikia asilimia 30.2 tu. Lakini amesema waliorodheshwa kupiga kura walifikia  asilimia 92.5.

Watu milioni 1,35 walishiriki katika kupiga kura. Kiongozi huyo Carrie Lam amesema kwa kupiga kura  wananchi hao wameunga mkono mfumo wa uchaguzi wa jiji lao. Wajumbe waliosimama kwenye  uchaguzi walichaguliwa na kamati ya China. Wapinzani na watetezi wa demokrasia wameukosoa uchaguzi huo kwa sababu wajumbe wao  hawakuruhusiwa kushiriki.

Vyanzo:/AFP/AP