Washirika Ulaya wataka kuimarisha sekta ya silaha ya Ukraine
14 Januari 2025Mawaziri wa ulinzi kutoka Poland, Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uingereza waliokutana mjini Warsaw jana Jumatatu wamekubaliana kuimarisha juhudi za kuijengea uwezo sekta ya silaha ya Ukraine hasa wakati huu inapopambana na Urusi.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema iwapo Ukraine itakuwa na uwezo wa kutengeneza silaha nchini humo, basi itakuwa rahisi zaidi kulihami jeshi lake kwa vifaa na silaha.
Soma pia: Mgogoro wa Ukraine na Urusi: Mashambulizi ya droni, diplomasia ya kimataifa, na mustakabali wa amani
Mawaziri hao pia wamejadili masuala ya usalama wa Ulaya katika muundo mpya wa ushirikiano wa mataifa matano uliobuniwa kufuatia ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais.
Rais huyo mteule wa Marekani ametishia kutozilinda nchi za jumuiya ya NATO ambazo zitakosa kuongeza bajeti zao za ulinzi hadi asilimia tano ya pato jumla la taifa.