1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa watano wa IS wakamatwa Sweden

4 Aprili 2023

Shirika la usalama wa taifa nchini Sweden llimesema maafisa wa usalama wamewatia mbaroni watu watano wanaoshukiwa kuwa magaidi wa kundi la Dola la Kiislamu

https://p.dw.com/p/4PgYJ
Pakistan Proteste gegen die Verbrennung eines Korans in Schweden
Picha: asif hassan/Agence France-Presse/Getty Images

Shirika la usalama wa taifa nchini Sweden llimesema maafisa wa usalama nchini humo wamewatia mbaroni watu watano wanaoshukiwa kuwa magaidi wa kundi la Dola la Kiislmu kuhusiana na maandamano baada ya tukio la kuchomwa Quran mwezi wa Januari.

Akizungumza na shirika la habari la TT, Susanna Trehörning, afisa msimamizi wa shirika hilo amesema wanachukulia kuna mafungamano ya kimataifa, hasa na kundi la kigaidi la dola la kiislamu. Wanaume hao watano walikamatwa katika operesheni zilizofanyika katika miji ya Eskilstuna, Linköping na Strängnäs.

Trehörning amesema tangu kuchomwa kwa Quran kumekuwa na ongezeko la vitisho dhidi ya Sweden na masilahi ya Sweden. Kwa mujibu wa tathmini ya shirika la Säpo hakuna kitisho kilichopo cha kufanyika shambulizi. Ofisi ya mwendesha mashitaka inatakiwa kuamua kufikia Ijumaa kama iwaweke rumande washukiwa hao watano.