1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Wasichana watatu wafariki baada ya boti la wahamiaji kuzama

10 Aprili 2024

Waokoaji katika kisiwa cha Mashariki mwa Ugiriki cha Chios, wamepata miili ya wasichana watatu waliofariki dunia baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kutoka Uturuki kugonga miamba.

https://p.dw.com/p/4edJF
Ugiriki
Watu 14 ikiwa ni pamoja na watoto wanane waliokolewa na walinzi wa Pwani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Chios Picha: Pau de la Calle/AP/picture alliance

Watu 14 ikiwa ni pamoja na watoto wanane waliokolewa na walinzi wa Pwani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa hicho kilichoko umbali wa kilomita 20 kutoka Uturuki.

Wanaume wawili pia walipatikana ufukweni mwa kisiwa hicho.

Maafisa wa kikosi hicho cha walinzi wa Pwani wanasema meli tatu za doria zinaendelea kutawatafuta manusura zaidi. 

Visiwa vya Ugiriki katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Aegean ni eneo maarufu la kuingia barani Ulaya kwa wahamiaji wanaotumia boti za wasafarishaji haramu kutoka Uturuki katika bahari hiyo inayolindwa na shirika la ulinzi wa mpakani la Umoja wa Ulaya, Frontex