UN: Tuna wasiwasi kuhusu ukandamizaji Venezuela
17 Septemba 2024Wamesema hayo katika ripoti mpya ya uchunguzi leo na kuongeza kwamba serikali ya Venezuela imeongeza matumizi ya nyenzo kali zaidi za hatari na zenye ukatili za ukandamizaji kufuatia uchaguzi wa rais wa mwezi Julai mwaka huu uliozozaniwa.
Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mnamo Julai 28 umekosolewa kwa kukosa demokrasia na ulionuaia kuendelea kumuweka madarakani rais Nicolas Maduro.
Soma pia:Mpinzani wa Rais Maduro akimbilia Uhispania, aahidi kuendeleza mapambano
Katika ripoti yake tume ya uchunguzi kwa ajili ya Venezuela, iliyopewa kazi hiyo na baraza la haki za binadamu linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa, imelaani ukiukwaji wa haki, ikiwemo kuwazuia watu bila kuwafungulia mashitaka, mateso na udhalilishaji wa ngono na mateso ya kijinsia yanayofanywa na vyombo vya usalama, ambayo kwa ujumla wake ni uhalifu dhidi ya ubinadamu wa mateso kwa misingi ya kisiasa.