1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu wasema visa vya mpox vinapungua

4 Novemba 2024

Maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasema visa vya maambukizi ya virusi vya mpox vinaonekana kupungua.

https://p.dw.com/p/4mZNR
DR Kongo | Chanjo ya mpox Kamanyola
Kampeni ya chanjo imeripotiwa kufanikiwa kwa aislimia 100 nchini DR Kongo.Picha: Ernest Muhero/DW

Baadhi ya maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema idadi ya visa vya maambukizi ya ugonjwa wa mpox inapungua hali inayotoa matumaini kwamba janga la kiafya linaelekea kudhibitiwa. 

Katika wiki za hivi karibuni, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeripoti maambukizi kati ya 200 hadi 300 yaliyothibitishwa na maabara kila wiki, tifauti na karibu visa 400 vilivyokuwa vikiripotiwa kila wiki mnamno mwezi Julai. Takwimu hiyo ni kulingana na shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO.

Soma pia: Makahaba, wachimba madini wachochea kusambaa kwa mpox Kongo

Idadi hiyo ya chini ya maambukizi imeshuhudiwa pia katika eneo la Kamituga, mji maarufu kwa machimbo ya madini mashariki mwa Kongo kulipoibuka kisa cha kwanza cha maambukizi hayo.

Wanasayansi bado wametoa mwito wa kuwepo utoaji chanjo kwa idadi kubwa zaidi ya watu kama njia ya kuzuia kabisa kusambaa kwa maradhi ya mpox. Kituo cha kuzuia na kudhibiti maradhi baraniAfrika, CDC, kimekadiria Kongo pekee inahitaji angalau dozi milioni 7 za mpox lakini hadi sasa ni dozi laki 9 pekee ndiyo zimeahidiwa kutolewa kwa nchi 9 za Afrika kutoka masharika ya hisani.