1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watafiti: Huenda vifo Sudan ni vingi kuliko inavyoripotiwa

14 Novemba 2024

Zaidi ya watu 61,000 wanakadiriwa kufariki duniani huko Khartoum katika miezi 14 ya kwanza ya vita vya Sudan.

https://p.dw.com/p/4myhc
Sudan
Watafiti wasema huenda vifo Sudan ni vingi zaidi ya vinavyoripotiwaPicha: AFP

Ushahidi wa ripoti mpya iliyotolewa na watafiti kutoka Uingereza na Sudan unaonyesha kwamba idadi ya waliofariki ni kubwa mno kuliko ilivyorekodiwa awali.

Makadirio hayo yanajumuisha watu 26,000 waliokufa vifo vya mateso, idadi hiyo ikiwa juu kuliko ile inayotumiwa na Umoja wa Mataifa kwa nchi nzima ya Sudan.

Sudan yaongeza muda wa kukifungua kivuko cha Adre

Ripoti hiyo pia inaonyesha kwamba ukosefu wa chakula na magonjwa ndiyo mambo yanayoendelea kuwa vyanzo vikuu vya vifo vinavyoripotiwa kote nchini Sudan.

Watafiti hao wanasema makadirio ya vifo kutokana na sababu zote katika jimbo la Khartoum ni asilimia 50 zaidi ya wastani wa kitaifa kabla kuanza kwa vita kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.