Watawala wa kijeshi Niger waomba msaada mamluki wa Wagner
5 Agosti 2023Wanajeshi hao wamepewa muda hadi kesho la sivyo nchi za jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS zitaingilia kati na ikiwezekana kijeshi. Mwandishi habari na mwanazuoni mwandamizi wa kituo cha Soufan, Wassim Nasr ameliambia shirika la habari la AFP kwamba maombi ya wanajeshi hao yamefahamika baada ya kiongozi mmoja wa watawala hao jenarali Salifou Mody kufanya ziara katika nchi jirani ya Mali.
Soma zaidi:ECOWAS wakubaliana uwezekano wa kuingilia kati kijeshi Niger
Kwa mujibu wa taarifa, wakuu wa ulinzi wa nchi za Afrika magharibi za jumuiya ya ECOWAS wamekamilisha mpango wa kuingilia kati nchini Niger. Wakuu hao wa kijeshi wamefikia uamuzi huo baada ya wasuluhishi wa nchi za ECOWAS kukataliwa kuingia katika mji mkuu wa Niger, Niamey au kukutana na kiongozi wa watawala wa kijeshi, Jenerali Abdourahmane Tchiani.