1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wa Asia Kusini wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji

13 Novemba 2023

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF imesema kwamba karibu watoto milioni 347 wa Kusini mwa Asia wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/4YjgE
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEFPicha: Denis Balibouse/REUTERS

Idadi hiyo ni zaidi ya nusu ya idadi jumla ya watoto wanaoishi kwenye ukanda huo na robo ya idadi ya watoto kote ulimwenguni.

Kulingana na ripoti hiyo, kiwango hicho cha asilimia 55 ni cha juu zaidi ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.

Asia ya Kusini yenye mataifa manane inakabiliwa na ongezeko la athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo ni pamoja na mafuriko na ukame.

Afrika Mashariki na Kusini yanalifuatia eneo hilo, likiwa na watoto milioni 130 wanaokabiliwa na changamoto kama hiyo.