1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wauawa Haiti

4 Oktoba 2024

Karibu watu 11 wameuwawa na dazeni kadhaa wengine kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa usiku wa kuamkia leo katika mji wa Pont-Sonde huko Haiti, ulio chini ya uongozi wa genge la wahalifu la Gran Grif.

https://p.dw.com/p/4lP5d
Kenya, Haiti
Askari wa Kenya ambaye ni sehemu ya kikosi cha kimataifa nchini Haiti.Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Haya yameripotiwa na gazeti la mji huo la Le Nouvelliste wakati ambapo magenge yaliyojihami yanapoendelea kutanua ushawishi wao mbali na mji mkuu.

Gazeti hilo linaripoti kuwa wanachama wa genge hilo linaloongozwa na Luckson Elan mwenye umri wa miaka 36 na ambaye aliwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, wameteketeza majengo na kuuwa watu mitaani.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waongeza muda wa kikosi cha polisi Haiti

Polisi ya kitaifa ya Haiti imeliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu kadhaa wameuwawa na kujeruhiwa bila kutoa idadi kamili.

Vyombo vyengine vya habari vimeripoti huenda dazeni kadhaa ya watu wameuwawa kutokana na mashambulizi hayo.

Maelfu ya watu wameukimbia mji huo wa Pont-Sonde ulioko kaskazini mwa Port-au-Prince na kukimbilia mji wa pwani wa Saint-Marc.