Watu 12 wauawa katika shambulizi la droni nchini Sudan
3 Aprili 2024Mkazi aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa njia ya simu, amesema kuwa moto ulizuka jana baada ya shambulio hilo lililotokea wakati wa mlo wa kufungua mfungo wa Ramadhani.
Wapiganaji wa kundi la Baraa na raia walikuwa wanashiriki mlo pamoja
Mkazi mwingine ameliambia shirika hilo la habari la AFP kwamba mlo huo uliokuwa umeandaliwa na wapiganaji wa itikadi kali wa Baraa wanaopigana pamoja na jeshi la nchi hiyo, uliwaleta pamoja raia na wapiganaji hao.
Soma pia:Juhudi hizo za upatanishi nchini Sudan bado zitaongozwa na Saudi Arabia na Marekani
Daktari wa hospitali moja katika eneo hilo la Atbara, amesema majeruhi wa tukio hilo pamoja na miili ya waliouawa, walifikishwa hosptalini humo bila ya kubainisha ikiwa walikuwa wapiganaji ama raia.
Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika katika shambulizi hilo.