1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 12 wauawa kufuatia shambulio la Israel Gaza

9 Januari 2025

Shirika la ulinzi la Gaza limesema kuwa watu wasiopungua 12 wameuawa wakiwemo wasichana watatu kufuatia shambulio la jeshi la Israel katika Ukanda wa huo.

https://p.dw.com/p/4oyUx
Watu wasiopungua 12 wameuawa wakiwemo wasichana watatu kufuatia shambulio la jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza
Watu wasiopungua 12 wameuawa wakiwemo wasichana watatu kufuatia shambulio la jeshi la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: BASHAR TALEB/AFP/Getty Images

Wasichana watatu na baba yao waliuawa baada ya shambulio la anga la Israel kuilenga nyumba yao katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katikati mwa Gaza.

Katika shambulio lingine tofauti, watu wanane waliuawa baada ya nyumba yao kushambuliwa katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa Gaza, sehemu ambayo jeshi la Israel limeelekeza oparesheni yake tangu Oktoba 7.

Mashambulizi hayo ya hivi karibuni yametokea wakati Qatar, Misri na Marekani zikiongoza mazungumzo mjini Doha, kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas ili kufikia makubaliano ya kumaliza mapigano Gaza yaliyodumu miezi 15.