Watu 15 wameuawa baada ya mashambulizi ya M23 nchini Kongo
5 Machi 2024Matangazo
Eneo hilo la mashariki mwa Kongo linakabiliwa na mgogoro huku maelfu ya watu wakilazimika kukimbilia usalama wao kutoka kwenye eneo hilo. Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya Kongo yamepamba moto katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Rutshuru na Masisi. Taarifa zaidi zinasema usafiri kuelekea Gomamji mkuu wa Kivu Kaskazini umekatishwa. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi zinaituhumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi hao wa M23 katika jitihada zake za kudhibiti rasilimali za madini. Serikali ya Rwanda inakanusha vikali madai hayo.