Watu 18 wameuwawa katika mashambulizi Burkina Faso
6 Februari 2023Matangazo
Duru za kiusalama zimethibitisha kutokea kwa shambulio lakini hazikutoa idadi ya waliouwawa.
Siku ya Jumamosi, wanajeshi sita waliuawa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, baada ya kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.
Kutetereka kwa hali ya usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi kunakosababishwa na makundi ya itikadi kali, kumezusha hasira ndani ya jeshi.
Burkina Faso ilishuhudia mapinduzi mara mbili katika 2022, ya mwisho yakiwa ya mwezi Septemba, wakati Kapteni Ibrahim Traore mwenye umri wa miaka 34 alipotwaa madaraka.