1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Watu 20 raia wa Haiti wafa baharini nchini Brazil

14 Aprili 2024

Watu 20 wanaodhaniwa kuwa raia wa Haiti wamekutwa wamekufa katika boti kaskazini mwa Brazil.

https://p.dw.com/p/4ejur
Mzozo wa wahamiaji kutoka Haiti
Wahamiaji kutoka Haiti pwakivuka mto kutoka Colombia kuingia Panama wakitaraji kuwasili hadi nchini Marekani.Picha: Ivan Valencia/AP Photo/picture alliance

Jeshi la polisi limesema miili ya watu hao ilikutwa ikiwa imeanza kuharibika na kusema inawezekana watu hao walikufa kutokana na kiu na njaa.

Msemaji wa jeshi hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waliarifiwa na wavuvi baada ya kuiona boti karibu na mji wa Braganca katika jimbo la Para, pwani ya kaskazini mwa Brazil.

Mkuu wa polisi ya shirikisho katika eneo la Braganca Alexandre Calvinho, amesema wanaamini kwamba miili hiyo ni ya wahamiaji wa Haiti na kuongeza kuwa kutafanyika uchunguzi zaidi ili kufahamu chanzo cha vifo na kuwatambua wahanga.

Haiti inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinaadamu pamoja na ukosefu wa usalama kutokana na mapigano ya magenge ya uhalifu.