1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 24 wafa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza wamesema mashambulizi ya anga ya Israel katika vitongoji viwili vya mji huo, yamewaua watu 24 na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4hOGX
Rafah
Wapalestina wakiwa wamebeba maiti ya ndugu aliyeuawa Picha: Jehad Alshrafi/Anadolu/picture alliance

Maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza wamesema mashambulizi ya anga ya Israel katika vitongoji viwili vya mji huo, yamewaua watu 24 na wengine kadhaa wamejeruhiwa.Qatar yaendeleza juhudi za upatanishi kati ya Israel na Hamas

Msemaji wa shirika la ulinzi wa raia wa Gaza Mahmud Basal, alisema watu wasiopungua 20 wamekufa katika shambulizi lililotokea katika kitongoji cha Al-Tuffah na wengine wanne wamekufa katika shambulizi jingine kwenye kambi ya wakimbizi ya Al-Shati.

Jeshi la Israel limedai kuwa ndege zake za kivita zilikuwa zikishambulia maeneo mawili ya miundombinu ya kijeshi ya Hamas katika mji wa Gaza. Jeshi hilo pia limethibitisha kifo cha raia mmoja wa Israel aliyeuawa katika mji wa Palestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Nalo Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu limeripoti vifo vya watu 22 waliouawa katika shambulizi la makombora, yaliyoharibu ofisi za shirika hilo huko Gaza.